UHUNI WA SAIDA KAROLI


Saida Karoli anajulikana kwa kuadhimisha urithi wake wa Kitanzania, na mtindo wake mara nyingi unaonyesha asili yake. Mara nyingi anavaa nguo za kitamaduni za Kiafrika, kama vile Kitenge au Ankara.

 

Karoli ameonekana mara nyingi akiwa amevaa nguo za stara zenye kuupa mwili uhuru. Nguo za kitamaduni za Kitanzania mara nyingi zina muundo wa  sketi, magauni au blauzi.  Hivyo kuleta muonekano wa kuvutia na wenye adabu. 

 

Saida Karoli mara nyingi huweka vito vikubwa na vya kuvutia. Hii inaweza kuwa ni vikuku vya kipekee, bangili, hereni, na kadhalika. Vito hivi vinaboresha muonekano wake kwa ujumla na kuongeza mguso wa kitamaduni. 

 

Mtindo wa Karoli unaonyesha ya kwamba kupendeza kunaendana na kujiamini. Dunia ya sasa imeghubikwa na ushawishi kutoka mataifa ya magharibi, kitu ambacho sio kibaya lakini hali hii itasababisha tamaduni zionekane kama ni kitu cha historia.

 

Lakini kupotea kwa historia ya sasa kutasababisha kuzaliwa kwa historia mpya.


***MWISHO***

Popular Posts