SHISHI BABY


 Jina lake kamili ni ZENA YUSUPH MOHAMMED kwa sasa ana miaka 36. Ni mwanamke wa kwanza kufikisha followers million 1 kwenye mtandao wa Instagram na ndie msanii anayekubalika na wengi nchini Tanzania. 


Mafanikio ya shishi baby yanaendana sambamba na mapambano yake. Aliajiriwa kwenye Hotel ya Peacock Kisha akakutana na Vincent Kigosi almaarufu Kama "RAY" ambaye alimuingiza kwenye uigizaji alafu then akaja kukutana na Q-Chief ambaye alimkutanisha na RUGE MUTAHABA wa Clouds Media Group. Ni hisstoria ndefu lakini sasa tunaisoma ndani ya sekunde chache. 


Mwaka 2016 akawa balozi wa DUME CONDOMS TANZANIA. na mwaka 2017 akazindua mgahawa wake wa SHISHI FOOD.


Tofauti Kati ya SHILOLE na wasanii wengine wa kike. 


Shilole ni kiongozi

Watu wengi wanafanya Mengi yanayo hitaji usimamizi. Hali hij ni tofauti kwa mtu Kama shilole ambaye anafanya Mengi kwa uthubutu wake mwenyewe.


Shishi ni mtu wa kuwaka.


Sote tunapenda kupendeza lakini kina watu Kama shilole ambao kukosea kwao kwenye maswala ya kuvaa ni nadra Sana. Anapendeza zaidi hususani akivaa abaya na hijab. 


Shilole ni mtu wa watu.


Ametokea chini sawa na wengi watu na pamoja na mafanikio aliyonayo bado anaishi maisha ya mwanamke mswahili. Naskia ashawah kumzingua Joti kisa alikuwa anamfanyia utani Sana. Pia nilishawahi kumuona akisukumana na Baba Levo kisa ubwabwa wa SHISHI food

Popular Posts