MISS TANZANIA


 Historia fupi.

 

Mwanamitindo wema alizaliwa 1990 [miaka 32 sasa], Mwaka 2006 alipata taji la Miss Tanzania. Mwaka 2010 alikuwa na mahusiano na Marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA, na baada ya huyo  akawa kwenye  mahusiano na DIAMOND PLATNUMZ. Wema na Mondi walikuwa deep sana kiasi kwamba mwaka 2011 Sepetu akatengeneza filamu ya “SUPERSTAR” ambayo iliongelea mahusiano yao wawili hao.

 

Wema na Fashion.

 

Zifuatazo ni sababu zinazo mtofautisha Wema na wengine kimtindo.

 

  • MWILI

Watu wa fashion tunaelewa ya kwamba mwili mzuri ndio utakaovutia zaidi. Miaka ya nyuma Sepetu alikuwa na mwili mkubwa wenye shape linalo eleweka na kuvutia. Siku hizi ana mwili mdogo wa mazoezi usioboa. Cha msingi ni kutokuwa na kitambi na mimafuta. Fanyeni mazoezi jamani.

 

  • NGOZI

Hii ni sawa na reception. Mara zote ngozi ya Sepet inagharamikiwa vitu vya bei ghali. Ukitaka kuvutia lazima uwe na ngozi flani hivi tamu kuliko asali ya mtume.

 

  • UBUNIFU

Ubunifu wa kupangilia mavazi ya mtoko ni swala la kuzingatiwa kiundani na mtu kama Wema Sepenga, hususani pale panapokuwaga na uwepo wa Fashion stylist wake. Martin Kadinda. Sometimes huwa anavaaga mavazi ya stara. Kama vile hijab kitu ambacho kina mheshimisha madame Wema na kumfanya aonekane ni mwanamke mstaarabu.  


***MWISHO***

Popular Posts